Mdee na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni ambaye pia ni Mbunge wa
Hai, Freeman Mbowe walitakiwa na Spika kuripoti kwenye Kamati hiyo kwa
kuwa walionesha vetendo vya utovu wa nidhamu.
Katika amri yake, Spika Ndugai alimtaka Mdee ambaye yupo nje ya mji
wa Dodoma kuwa amewasili mjini hapa hadi kufikia saa 4.23 asubuhi leo
ili kukutana na kamati hiyo vinginevyo Jeshi la Polisi limkamate popote
pale alipo na afikishwe Dodoma akiwa amefungwa pingu.
Akizungumza baada ya kuwasili mjini Dodoma, Mdee alisema tayari
ameshachukua samansi yake na yuko tayari kuripoti katika Kamati hiyo na
kukabiliana na tuhuma zinazomkabili.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasilaino ya
Bunge, Owen Mwandumbya, kamati hiyo ambayo ilikuwa ikutane nao jana,
iliahirisha hadi leo kwa kile alichoeleza kwamba wabunge wanaounda
kamati hiyo walikuwa katika shughuli nyingine za Bunge.
Spika alitangaza hayo bungeni juzi wakati akitoa majibu ya miongozo
iliyoombwa na Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM) na Mbunge wa Madaba,
Joseph Mhagama (CCM) ambao wote waliomba mwongozo kujua Spika anasemaje
kuhusu vitendo vya utovu wa nidhamu uliofanywa na wabunge hao.
Mbowe na Mdee wanadaiwa kufanya vitendo hivyo wakati na baada ya
kumalizika kwa uchaguzi wa wagombea wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA)
uliofanyika Aprili 4, mwaka huu.
chanzo:Habarileo.
Comments