Mbowe atishia kuipandisha CCM mahakamani.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman MboweMwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema wanajiandaa kufungua kesi mahakamani ili kupinga matokeo baada ya Wagombea waliopendekezwa na CHADEMA kukoseswa nafasi hiyo.
Wagombea ambao wamewakilishwa na na CHADEMA kuwania kuiwakilisha Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki ni Ezekiel Wenje na Lawrence Masha ambao walipigiwa kura nyingi za HAPANA jambo ambalo linaaminika ni mipango ya CCM.
Mbowe ameeleza kuwa wanafahamu hizo ni mbinu zilizofanywa na CCM dhidi yao na kusema kuwa zimetiliwa nguvu na zina baraka za Rais Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ili CHADEMA wasipate nafasi hiyo.

chanzo:zanzibar24.

Comments