Akizungumza kwa simu Jumamosi iliyopita, Mbatia alikiri kumwahidi
Mrema sukari, lakini akaomba apewe muda wa wiki moja kutimiza ahadi
yake.
Akizungumzia afya yake iliyosababisha asionekane jimboni na
bungeni, alisema kwa sasa afya yake imeimarika na hivi karibuni ataanza
kuonekana jimboni kwake akitekeleza majukumu yake.
Hatua ya Mbatia
inatokana na hivi karibuni Mrema kumshitaki kwa wananchi kuwa ameshindwa
kutekeleza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni mwaka juzi.
Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCRMageuzi kitaifa, alichukua
nafasi ya Ubunge wa Vunjo baada ya kumshinda Mrema katika Uchaguzi Mkuu
wa 2015.
Kwa mujibu wa Mrema, Mbatia alisema katika kipindi hicho kuwa
atafanya kila linalowezekana kuhakikisha miundombinu ya jimbo hilo
inakuwa sawa, lakini hilo hajatekeleza ahadi hiyo.
Kadhalika, Mrema alisema Mbatia amekuwa haonekani bungeni kwa kipindi
kirefu kupeleka kilio cha wananchi. Aliwataka wananchi wa Jimbo la
Vunjo kutathmini kauli aliyoitoa Mbatia kuwa yeye Mrema ni mgonjwa ili
wasichague kuwa mbunge.
Mrema alihoji ugonjwa unaomsumbua Mbatia na
kumfanya asishiriki shughuli za maendeleo jimboni kwake wakati yeye
Mrema anashughulikia kazi alizopewa na Rais John Magufuli bila ya
wasiwasi.
Mrema ambaye pia ni Mwenyekiti Bodi ya Parole aliyasema hayo
wakati akizungumza na wananchi kijijini kwake Kiraracha mkoani
Kilimanjaro hivi karibuni.
chanzo:Habarileo
Comments