
Urusi ilikuwa imekiri awali kuhakikisha kuwa hifadhi ya silaha za sumu, imeharibiwa kabisa - na kwa kushindwa kufanya hivyo, kulichangia kutokea kwa shambulio hilo baya, alisema.
Mawaziri wa nchi za kigeni wa mataifa yenye nguvu za kiuchumi duniani- G7, wanajiandaa kukutana baadaye leo Jumatatu huko Italia.
Mazungumzo hayo yatalenga namna ya kuongeza shinikizo kwa Urusi kujitenga na Rais wa Syria Bashar Al-Assad.
Mnamo siku ya Jumanne, Bw. Tillerson, ataendeleza mkutano huo wa G7 na kuwelekea Moscow, ambapo atakutana na waziri mwenzake wa mashauri ya nchi za kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov.
Urusi ni mshirika wa karibu wa serikali ya Syria, na alisaidia kuwezesha muafaka wa mwaka 2013, wa kuharibu zana za sumu za Syria.
Shambulio lililoshukiwa kuwa la sumu, lilitokea mjini Khan Sheikhoun, Jumatano iliyopita na kusababisha vifo vya watu 89.
Ili kujibu shambulio hilo, Marekani ilirusha makombora 59 yaliyolenga kambi za wanajeshi wa anga wa Syria.
chanzo:Bbc.
Comments