
"Iran isipochukuliwa hatua inaweza kwenda njia sawa na ya Korea
Kaskazini na kuubeba ulimwengu wote katika safari hiyo," Bw Tillerson
amesema.
Rais Donald Trump tayari ameagiza utathmini mpya ufanywe
kuhusu mkataba uliotiwa saini kati ya nchi za Magharibi kuhusu mpango wa
nyuklia wa Iran.
Hata hivyo, Marekani imekiri kwamba Tehran inatii makubaliano hayo ya mwaka 2015.
Iran kufikia sasa haijasema lolote kuhusu tamko hilo jipya kutoka kwa Marekani.
Iran imekanusha mara kwa mara tuhuma kutoka kwa nchi za Magharibi kwamba inajaribu kustawisha silaha za nyuklia.
Jumanne,
Marekani iliituhumu Korea Kaskazini na kusema taifa hilo lilikuwa
linajaribu kufanya "uchokozi kutokee jambo fulani", baada ya nchi hiyo
kufanya jaribio la kombora ambalo lilifeli mwishoni mwa wiki.
Kuijibu Marekani, Korea Kaskazini ilisema inaweza kuwa ikifanya majaribio ya makombora kila wiki.
Aidha, ilionya kwamba itaikabili Marekani kwa vita vikali iwapo taifa hilo litathubutu kuishambulia kijeshi.
Jumatano,
Bw Tillerson alsiema utathmini huo mpya kuhusu Iran, ambao aliutangaza
katika Bungela Congress siku moja awali, kando na kutathmini iwapo
Tehran imetimiza makubaliano ya mkataba huo wa nyuklia pia utachunguza
vitendo vya Iran Mashariki ya Kati.
Bw Tillerson aliituhumu Iran kwa kuhujumu juhudi za Marekani nchini Lebanon, Iraq, Syria na Yemen.
"Mpango
wa kina wa sera kuhusu Iran unatuhitaji tuangazie vitisho hivi
vinavyoletwa na Iran, na ni wazi kwamba ni vingi (vitisho)," alisema.
Bw Tillerson awali alikiri kwamba Iran ilikuwa
imeheshimu makubaliano ya mkataba huo wa 2015, lakini aliibua wasiwasi
kuhusu taifa hilo akisema limeendelea kuwa "mfadhili wa ugaidi".
Rais Trump kwa muda mrefu amekuwa akisema mkataba huo kuhusu Iran "ndio mbaya zaidi kuwahi kutiwa saini".

chanzo:Bbc.
Comments