
Awali maafisa wa Marekani walisema wana mpango wa kuchukua hatua za
kijeshi baada ya Syria kushutumiwa kutumia silaha za kemikali katika
mji unaodhibitiwa na waasi, ambapo watu kadhaa wamepoteza maisha.
Mashambulizi hayo yametekelezwa kutoka kwenye meli za kijeshi za Marekani katika bahari ya Mediterranea.

Naye mshirika wa Syria Urusi ametahadharisha madhara
yatokanayo na hatua zozote za kijeshi zinazochukuliwa na Marekani dhidi
ya Syria .
Hata hivyo Rais Donald Trump amsema kuwa ,kutumia gesi hatari kuua
raia wakiwemo watoto wengi, utawala wa Syria ulikuwa umevuka mipaka.
Mike Pregent ni mchambuzi wa masuala ya mashariki ya kati ameiambia BBC kuwa mashambulizi hayo yametoa ujumbe mzito kwa Assad.
Shambulio
hilo linawapa Watu wa Syria matumain, na ninachomaanisha ni kuwa haya
hakika haya ni Mashambulizi dhidi ya vikosi vya anga vya Assad, silaha
za kemikali, pengine dhidi ya hifadhi za mafuta halikadhalika.hivyo
haikuwa dhidi ya raia, haikuwaweka marubani wa kimarekani hatarini.

chanzo:Bbc.
Comments