
Kufutwa kazi kwa Gordhana kumesababisha masoko ya hisa kushuka kwa asilimia 5.
Bwana Gordhan alionekana kama mpinzani mkubwa wa ufisadi kwenye uongozi ambao umekosolewa vikali.
Aikuwa mmoja wa mawaziri waliofutwa kazi wakati Rais Jacob Zuma, alilifanyia mabadiliko baraza la mawaziri.
Bwana Ramaphosa alikiambia kituoa cha habari cha SABC kuwa
hatajiuzulu kufuatia kufutwa kwa mawaziri hao bali ataendelea
kuwatumikia watu.
Pravin Gordhan alitajwa na wengi kama mtu mwenye tajriba ya kusimamia uchumi.
Alikuwa akizuia matumizi makubwa ya serikali na kukataa wito wa rais wa kutaka matumizi ya serikali kuongezwa.
Huu ndiyo duru ya pili bwana Gordhan anahudumu kama waziri wa fedha baada ya kuhudumu kwanza kati ya mwaka 2009 na 2014.

chanzo:Bbc.
Comments