Hayo yalisemwa Arusha na Kaimu Jaji Mkuu, Profesa Ibrahimu Juma
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea mafunzo ya majaji wa
mahakama ya Rufaa, Majaji Wafawidhi na Majaji wa mahakama kuu
waliokutana Jiji Arusha kutathimini utendaji kazi wa mahakama na
kuboresha katika mwaka ujao.
Kaimu Jaji Mkuu alisema mapema mwaka 2014 kulikuwa na Majaji 90 kote
nchini na ufanisi katika kazi ulikuwa mzuri na msongamano wa kesi
mahakama kuu haukuwa mkubwa lakini majaji hao wengi wao walistaafu na
kufikia idadi ya Majaji 75 mwaka 2015.
Jaji Mkuu alizungumzia namna ya ilivyojipanga kuhakikisha kila mkoa
kote nchini unakuwa na mahakama Kuu na makama za mwanzo zinajengwa
katika kila tarafa au kata lengo ni kutaka kuona msongamano wa kesi
unamalizika kote nchini kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu.
Alisema fedha ziko kwani Benki ya Dunia na serikali imetoa fedha
nyingi kwa ajili ya uboreshaji wa mahakama zilizopo na kujengwa nyingine
zenye hadhi.
Akizungumzia kupotea kwa majalada ya kesi za watu na kutotolewa kwa
hukumu kwa wakati kuwa ni malalamiko makubwa ya wananchi dhidi ya
mahakama kwani yanajenga hisia kuwa ili upate vitu hivyo kwa wakati ni
lazima utoe rushwa.
chanzo:Habarileo.
Comments