Taarifa iliyotolewa na Takukuru Dar es Salaam iliwataja waliofikishwa
mahakamani kuwa ni mmiliki na Mganga Msaidizi Mfawidhi Kliniki binafsi
ya Basalia, Job Mwita Giryago na Mganga Msaidizi Mfawidhi Kituo cha Afya
cha serikali Kiagata Marcelina Narkiso Magana.
Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani jana mbele ya Hakimu Mkazi
Janeth Msaloche wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mara na kusomewa mashtaka
matatu ya rushwa na mwendesha mashtaka wa Takukuru William Fussi.
Katika shitaka la kwanza washtakiwa wamedaiwa kuwa katika tarehe
tofauti kati ya Januari na Februari, mwaka huu walipokea rushwa ya Sh.
350,000 kutoka kwa mgonjwa Nyabwire Mwikabe ili afanyiwe upasuaji katika
Kituo cha Afya Kiagata.
Katika shitaka la pili washtakiwa wamedaiwa kuwa katika tarehe
tofauti kati ya Januari na Februari, mwaka huu walipokea rushwa ya Sh.
350,000 kutoka kwa mgonjwa Justine Matinde ili afanyiwe upasuaji katika
Kituo cha Afya Kiagata.
Katika shitaka la tatu washtakiwa wamedaiwa kuwa katika tarehe
tofauti kati ya Januari na Februari, mwaka huu walipokea rushwa ya Sh.
350,000 kutoka kwa mgonjwa Spora Juma ili afanyiwe upasuaji katika Kituo
cha Afya Kiagata.
Mbali na mshitakiwa wa pili Marcelina Magana kukana mashitaka yote
matatu mshtakiwa wa kwanza Job Giryago hakuwepo mahakamani wakati shauri
dhidi yao lilipofunguliwa na kusomwa.
Upande wa Mashtaka uliiambia Mahakama kuwa uchunguzi wa shauri
umekamilika na uliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutaja shauri kwa
vile mshtakiwa wa kwanza hajafikishwa mahakamani.
Kesi imeahirishwa hadi Aprili 13, mwaka huu itakapotajwa tena na
Magana yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya
kuwa kuwa na wadhamini wawili waliosaini bondi ya Sh milioni 5, kila
mmoja.
chanzo:Habarileo.
Comments