Mabaraza ya Vijana Wilaya yatakiwa kubuni mbinu na miradi ya maendeleo.

wilayaBaraza la Vijana Taifa upande wa Zanzibar  limeyataka Mabaraza ya Wilaya kubuni mbinu na miradi ya maendeleo ambayo itaweza kuwasaidia katika kuendesha shughuli  zao ambapo itaepusha  kutegemea viongozi.

Wakizungumza katika Ziara maalumu ya kuyakagua mabaraza hayo ya Wilaya ya kaskazini A na B wamesema  ili kujikwamua na  hali gumu ya maisha kwa vijana lazima wabuni miradi  mbalimbali ikiwemo kilimo,Uvuvi,Ufugaji,Ushoni ambayo  itaweza  kuwanyanyua  na kuwapatia ajira za uhakika.
 
Hata hivyo wamesema lengo la kushajihisha mabaraza hayo kubuni miradi ni kwamba Serikali inamipango ya kuyainua mabaraza hayo kuanzia ngazi ya Taifa, Wilaya hadi Shehia  kwa kuyapatia mikopo itayoweza kuendesha  miradi  yao waliyoibuni.
 
Nao Viongozi wa Mabaraza ya Vijana ya Wilaya wamesema  licha ya kuchukua hatua  za kubuni  miradi lakini bado wanarudisha nyuma na baadhi ya vijana kutokuwa na utayari katika kujitolea kuendesha shughuli za  mabaraza na badala yake huyaona mabaraza hayo ni uwanja wa siasa.
 
Jumla ya Million mia 300 zimetengwa kwa ajili ya mabaraza ya vijana Zanzibar kwa Aajili ya kuendesha shughuli zao za maendeleo.
chanzo:Zanzibar24

Comments