Waandamanaji walikusanyika katika miji mikuu nchini humo wakitaka
rais huyo kujiuzulu baada ya kufutwa kazi kwa waziri aliyeheshimiwa wa
fedha.
Vikundi vya watu vilikusanyika kabla ya maandamano hayo katika miji ya Johannesburg, Cape Town, Durban na mji kuu wa Pretoria.
Hatua ya Zuma kumfuta kazi waziri wa fedha Pravin Gordhan ilisababisha kukatwa kwa kiwango cha mkopo nchini humo.
Mwelekeo huo uliongezea shinikizo kwa uchumi wa Afrika Kusini ambao umekumbwa na utata.
Maelfu ya watu walitarajiwa kuandamana na picha ambazo zilisambazwa
katika mitandao ya kijamii siku ya Ijumaa zikionyesha vikundi vikubwa
vya watu nje ya bustani ya makanisa mjini Pretoria, ijapokuwa kulikuwa
na hali ya ati ati ya iwapo maandamano hayo yalikuwa halali.
Polisi
walisema siku ya Alhamisi kuwa maandamano mjini Pretoria sio halali
kwasababu hawakuwa wamepewa kibali na mamlaka ya mji.
Lakini baadaye hatua hiyo ligeuzwa na hakimu.

Mamia ya wakongwe
waliopigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na vijana walio wanachama wa
chama kinachotawala walizingira nje ya makao makuu ili kulinda majengo
yao.
Serikali ambayo ilitoa mwito wa amani wakati wa maandamano
hayo yaliyofanyika nchi nzima, iliandika katika mtandao wake wa twitter
kuwa sharia za Afrika Kusini hulinda maslahi ya wote ikiwemo pia wale
ambao hawakutaka kujiunga na maandamano.
Mapema katika wiki, kamati ambayo hufanya maamuzi makubwa ndani ya
chama cha ANC ilitupilia mbali malalamishi dhidi ya Zuma kuwa
hakuwasiliana na watendaji wakuu kabla ya mabadiliko ya baraza la
mawaziri.

Iliwaacha baadhi ya viongozi wa ANC wakitia shaka iwapo Zuma anastahili kubaki kama rais.
Washirika
wakuu wa ANC, chama cha South African Communist Party (SACP) na vyama
vikuu vya wafanyikazi (Cosatu) waliunga mwito wake kutimuliwa.
Lakini kamati ya chama (NWC), ikijadiliana kuhusu mabadiliko katika baraza la mawaziri, baadaye ilimuunga mkono rais.

chanzo:Bbc.
Comments