Ikiwa
leo Tanzania inatimiza miaka 53 toka Tanganyika na Zanzibar
zilipoungana mwaka 1964 na kuunda nchi ya Tanzania Mbunge wa jimbo la
Mtama, Mh Nape Nnauye amefunguka na kusema CCM ndiyo waasisi wa Muungano
huo.
Mhe
Nape Nnauye anakiri kuwa licha ya mapungufu ya hapa na pale katika
chama chake hicho lakini bado kinabakia kuwa chama bora cha mfano barani
Afrika, Nape Nnauye amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter.
"CCM
bado ni Chama bora cha mfano kwa Afrika! Ni imara na kina historia
ndefu, nzuri iliyotukuka sana! Ndio waasisi wa Muungano Wetu,
tuudumishe" alisisitiza Nape Nnauye
chanzo:mpekuziblog.
Comments