Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Zanzibar asmema kuna umuhim wa kuunda mipango kazi katika baraza hilo.

Amesema bila ya baraza la Vijana kutayarisha mpango kazi shughuli mbali mbali za maendeleo ya vijana hayatakuepo.
Ndugu Khamis aliyasema hayo leo asubuhi huko kwenye ukumbi wa
mikutano wa Skuli Ya Madungu Sekondari alipokuwa akifungua mkutano wa
baraza la vijana huko Pemba wa kuandaa mpango kazi wa baraza hilo.
Amesema mpango huo utatoa ajira kwa baraza na vijana ili waweze
kufanya kazi kwa uhakika na kwa ufanisi katika masuala ya kiuchumi,
kijamii na kiutamaduni.
Aidha Katibu mtendaji wa baraza la vijana Zanzibar amefahamisha
kwamba mpango huo utawawezesha vijana kunufaika na fursa zilizopo na
kuwa na uwezo wa kuibua fursa nyengine.
Mkutano huo uliowashirikisha wajumbe wa mabaraza ya vijana wa ngazi
mbali mbali huko Pemba pia mkutano kama huo ulifanyika jana huko katika
Kisiwa cha Unguja.
chanzo: zanzibar24.
Comments