Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu hatari ya kupanuka zaidi udhibiti wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika maeneo mbalimbali ya Libya na hali mbaya inayotawala maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo.
António Guterres amesema kuwa, ana wasiwasi kuhusu harakati zinazoshadidi na ukatili mpya unaofanywa na wanachama wa kundi hilo nchini Libya na vilevile mkwamo wa kisiasa unaoshuhudiwa nchini humo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, licha ya kuwa kundi la Daesh halidhibiti kikamlifu eneo lolote la Libya lakini wanachama wake wanaendeleza harakati zao katika ardhi ya nchi hiyo na wanaendelea kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali.
Kundi la kigaidi na kiwahabi la Daesh Julai 2015 lilivamia na kuteka miji mingi ya Libya kutokana na ombwe wa kisiasa na kiutawala unaoendelea kuisumbua nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Comments