Akizungumza huko katika eneo la ujenzi huo Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mwakilishi wa jimbo la Fuoni Mh Yussuf Hassan Idd amewataka wasimamizi kuongeza bidii na kama kuna changamoto zinazorudisha nyuma kazi hiyo waziweke wazi ili kuchukuliwa hatua.
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa majengo hayo Mbarouk Mussa Mbarouk ameieleza kamati hiyo kwamba kazi iliyokwishafanyika ni asilimia 25% kwa miezi sita na hii imetokana na ugumu uliosababishwa na uchimbaji wa misingi ya usimamishaji wa majengo hayo.
Aidha mshauri huyo amesema kuwa kuna mabadiliko ya ziada yaliyojitokeza ya kujengwa ghorofa tatu badala ya mbili za awali.
Naye Afisa Mdhamini wizara ya Fedha na mipango Pemba Ibrahim Saleh Juma ameishukuru kamati hiyo kwa kutembelea maeneo hayo na kuona maendeleo na harakati za ujenzi zinazoendelea
chanzo:zanzibar24.
Comments