Jaji Juma alisema hayo jijini Arusha alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari katika mafunzo ya siku tano yaliyohusisha Majaji wa
Mahakama ya Rufaa, Majaji Wafawidhi na Majaji wa Mahakama Kuu namna ya
kuboresha utendaji kazi wa mahakama.
Alisema mwenye mamlaka ya kutafsiri hukumu ama maamuzi ya mahakama ni
Msajili wa Mahakama Kuu wa Kanda husika au mahakama na sio mtu mwingine
yeyote.
Kaimu Jaji Mkuu alisema kuwa kinachofanyika sasa kwa wanasheria wa
serikali na binafsi na wanasiasa kuzungumza na waandishi katika viwanja
vya mahakama na kutafsiri kilichoamriwa na mahakama ni kuingilia uhuru
wa mahakama na hakipaswi kufanyika tena.
chanzo:Habarileo.
Comments