Rais John Magufuli leo ametoa msamaha kwa wafungwa 2,219 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Projest Rwegasira inaeleza kuwa wafungwa hao ni wale wenye magonjwa kama Ukimwi, saratani na Kifua Kikuu na wazee wenye umri wa kuanzia miaka 70.
Comments