Jeshi la Polisi la Mkoa wa Mjini Magharibi latoa ta hadhari kwa wakaazi wa mabondeni.

polisiJeshi la Polisi la Mkoa wa Mjini Magharibi  limewataka wakaazi wa maeneo ya mabondeni kuwa na tahadhari kubwa katika kipindi hichi cha mvua za masika ili kujinga na majanga yanayoweza kujitokea ikiwemo kuharibika kwa nyumba na mali zao.
Akizungumza na Mwanahabari wetu huko ofisini kwake Muembe Madema  Kamanda wa Polisi wa mkoa huo Hassan Nassir amesema mbali na taasisi za serikali kuwa na jitihada za kuwaelimisha jamii juu ya kuhama katika maeneo ya mabondeni lakini baadhi yao wamekuwa hawafuati elimu hiyo.

Hata hivyo amesema katika kukabiliana na majanga yatokanayo na mvua  ni vyema kwa wananchi kuacha kujenga maeneo yanayotuama maji ya mvua pamoja kuwakataza watoto wao kucheza katika sehemu zinazotuama maji wakati mvua ikiendelea kunyesha.
Akizungumza suala la usalama wa Barabarani kamanda Nassir ametowa wito kwa waendesha vyombo vya moto kufuata sheria ziliwekwa na kucha tabia ya kuendesha vyombo vya moto wakati wakiwa wamelewa ili kujiepusha ajali zisizo za lazima hususan katika kipindi cha mvua.
chanzo: Zanzibar24.

Comments