
Katika mkutano wake na waandishi wa habari Kamishna Sirro alisema
lengo la kuimarisha ulinzi kipindi cha Sikukuu ya Pasaka ni kuhakikisha
wananchi wa jiji hilo wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu
kwa kuwa uzoefu unaonesha kuwa mara nyingi kipindi cha sherehe watu
wenye nia ovu hujiandaa kufanya vitendo vya kihalifu.
Aliongeza kuwa askari polisi watafanya doria za miguu na magari
katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha vitendo vyote vya kihalifu
vinadhibitiwa.
“Jeshi la Polisi Kanda Maalumu limejipanga kwa namna nyingi, ikiwa ni
kufanya doria za saa ishirini na nne katika maeneo yote ya jiji hasa
maeneo yenye viashiria vya uhalifu, pia patakuwa na doria maeneo ya
makanisani, Kumbi za starehe na maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya
watu,”alisema Kamanda Sirro.
Sambamba na hilo, askari kanzu pamoja na Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), mbwa na farasi pamoja na vikosi vyote.
“Jeshi la Polisi linawaomba wakazi wa jiji kuonesha ushirikiano kwa
kutambua kuwa jukumu la kuzuia uhalifu ni la kila mmoja wetu, hivyo
washiriki kutoa taarifa za uhakika za kihalifu ili kuhakikisha hatua
zichukuliwe haraka kabla madhara hayajajitokeza.”
chanzo: zanzibar24.
Comments