Mhagama alisema hayo juzi wakati alipotembelea kiwanda cha kusindika
nyama cha Nguru Hills Ranch kilichoko wilayani Mvomero, mkoa wa
Morogoro.
Alisema uwekezaji katika viwanda utaongeza kiwango cha
asilimia ya Watanzania watakaojiunga na mifuko ya hifadhi za jamii na
kufanikisha kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira ambacho kwa sasa
kimeshuka kutoka asilimia13 hadi kufikia asilimia 10.3.
Waziri Mhagama aliambatana na Naibu wake, Anthony Mavunde na kupokewa
kiwandani hapo na Uongozi wa Serikali ya Mkoa wa Morogoro ukiongozwa na
mkuu wa mkoa huo, Dk Kebwe Stephen ambaye alifuatana na mkuu wa wilaya
ya Mvomero, Mohamed Utaly na watendaji wengine wa serikali ya wilaya na
mkoa wakiwemo viongozi wa Kijiji cha Wami Sokoine.
Hata hivyo, alisema
ziara hiyo ililenga kufuatilia maelekezo aliyoyatoa Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa alipofanya ziara mkoani Morogoro, Agosti 3, mwaka 2016 na
kukitembelea kiwanda hicho ambapo moja ya changamoto iliyojitokeza ni
ukosefu wa fedha za ukamilishaji kabla ya kuanza uzalishaji wake.
Alisema kutokana na mazungumzo yaliyofanyika mapema mwaka huu, Mfuko
wa Pensheni wa LAPF umefikia uamuzi kutoa fedha za kuwekeza kwenye
kiwanda hicho ili kumalizika kazi zilizobaki na kukiwezesha kufanya kazi
za uchinjaii wa ng’ombe na mbuzi ikiwa na kutoa ajira kwa wananchi
miezi sita ijayo mwaka huu.
Waziri Mhagama alisema kuwa, Mfuko wa LAPF
utawekeza fedha katika kiwanda hicho kulingana na utaratibu wa kisheria
utakaosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi
ya Jamii (SSRA) ili kuona fedha za wanachama zinaingizwa kwenye
uwekezaji ulio salama na wenye kuleta faida kwa mfuko na serikali.
Hata hivyo, waziri huyo alisema kuwepo kwa kiwanda cha kuchakata
nyama wilayani Mvomero mkoani Morogoro kitamaliza mgogoro wa muda mrefu
kati ya wakulima na wafugaji kwa kuwa wafugaji watapata fursa ya kuuza
mifugo yao kiwandani hapo na wakulima kuzalisha nyasi za malisho.
Kwa
upande wake Mkurugenzi na Mshauri wa Kiwanda cha Nguru Hills Ranch,
Dunstan Mrutu alisema kiwanda hicho chenye uwezo wa kuchinja ng’ombe
300, mbuzi na kondoo 1,500 kwa siku kutokana na uwezeshaji wa fedha
kutoka LAPF kitatarajiwa kufunguliwa ndani ya miezi sita ijayo mwaka
huu.
Mkurugenzi huyo alisema takriban asilimia 80 ya nyama itakayochinjwa
kiwandani hapo itafungashwa na kuuzwa nje ya nchi, hasa Uarabuni kwa
sababu nyama ya mbuzi ya Tanzania imebainika kuwa na mvuto maalumu
katika nchi hizo.
Alisema nia yao ni kuitikia mwito wa Rais John
Magufuli wa kutaka viwanda vizalishe viatu nchini kuanzia vya majeshi na
wananchi wote ambapo wamepanga kuanzia mwakani wataanza kuuza bidhaa
hizo.
chanzo:habarileo.
Comments