Hatuwezi kujenga Demokrasia ikiwa waandishi wahabari hawafanyi kazi yao katika hali ya amani.

waandishiMwenyekiti wa chama cha wananchi CUF anayetambulika na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba amesema analaani kitendo cha kupigwa waandishi wa habari na jimbo amabalo asilo likubali kabisa na ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo lililo tokea  April 22, 2017 Jumamosi majira ya Saa 5  katika Hoteli ya Vina Mabibo jijini Dar es Salam.

Lipumba ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa habari wa Azam Two na alisema kuwa hatuwezi kujenga Demokrasia ikiwa waandishi wahabari hawafanyi kazi yao katika hali ya amani na utulivu.
“Baada ya kulisikia hilo niliamua kuchukua jukumu la kuwaandikia Jukwaa la wahariri barua ambayo ipo mbioni kwenda kwenye ofisi zao kwamba mimi binafsi kama mwenyekiti wa CUF nalaani kitendo cha kupigwa kwa waandishi wa habari na nijambo ambalo hatulikubali kabisa, hatuwezi kujenga Demokrasia ikiwa waandishi wahabari hawafanyi kazi yao katika hali ya amani na utulivu” alisema lipumba.
“Vile vile kijana wetu amekatwa kisigino kwa panga na anavyo elewa yeye kijana aliyemkata anaitwa Mohamedi Mgonvi na taarifa hii imepelekwa kwenye vyombo vya dola kwaiyo vyombo vya dola inalishughulikia na tulitoa wito ambao ulitolewa na Mkurugenzi wetu wahabari na uwenezi”
Aidha  Prof. Lipumba ameeleza kuwa toka awali ametaka kumaliza tofauti zakisiasa katika chama chao na kumtaka  Maalim kwenda katika ofic za buguruni kwa mazungumzo.
“Mimi toka awali nimeeleza kwamba nataka tumalize tofauti za kisiasa kwa mazungumzo tupate suluhu tuheshimu katika ya chama chetu na nimekuwa nikimuita Maalim Seif aje ofisi buguruni aweze kuzungumza afanye kazi zake kama katibu mkuu na mimi nimemfahamu Maalim Seif mwaka 1973 tukiwa wanafunzi wa chuo kikuu Dar es Salaam kwahiyo hatuna sababu ya sisi kuwa na mgogoro huu na kuuruhusu kuendelea”.
“Hivi sasa kupitia taarifa zetu zakiuchunguzi zinaonesha kwamba kuna mbinu yakutaka chama hiki kiweze kufutwa kwaiyo kuna matukio ya napangwa njee ya chama ili paweze kutokea vurugu nazikishatokea waseme chama hiki hakifai kuendelea kuwa chama cha siasa na utakuta kuna vyama vingine vya siasa vinashabikia na kutoa wito ilichama hichi kiweze kufutwa” Prof. Lipumba.
chanzo:zanzibar24.

Comments