Mbunge
wa jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Halima Mdee jana amefunguka
na kuomba radhi bungeni kufuatia kutoa lugha isiyokuwa na staha bungeni
wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika
April 4, 2017.
Halima
Mdee wakati akiomba radhi hiyo anasema kuwa siku hiyo ya uchaguzi
kulikuwa na matukio ambayo yalikuwa yakiendelea bungeni ambayo
yalimpelekea kutoa lugha isiyokuwa sawa kitamaduni za bunge, ambayo
ilimgusa Spika wa Bunge na Naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kigwangala
"Mhe.
Mwenyekiti tarehe 4 mwezi wa 4 wakati wa uchaguzi wa EALA kuna matukio
ambayo yalikuwa yanaendelea yakanipelekea kuzungumza lugha ambayo
kitamaduni za Bunge si sawa na lugha husika ilimgusa Spika wa bunge na
Mhe, Kigwangala kwa namna moja au nyingine
"Kama
mbunge mzoefu nilitumia jitihada binafsi kuzungumza na kuomba radhi
wahusika katika 'individual capacity'lakini vilevile nikaona ni busara
kwa sababu haya maneno niliyasema bungeni hivyo kuzungumza pia hapa na
kumuomba radhi Mhe. Spika kwa hiyo niliomba huu muda kwa lengo la
kumuomba radhi, kumwambia namuheshimu na kumwambia sitarudia" alisema Halima Mdee
Mbali
na hilo Halima Mdee aliendelea kuomba radhi kwa wabunge, watanzania
pamoja na wananchi wa jimbo la Kawe lakini pia Halima Mdee alisisitiza
kuwa michango yake ya bunge itaendelea kama kawaida yake lakini kwa
kutumia lugha za staa.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments