
Wakili wa Serikali, Joseph Maugo alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi,
Godfrey Mwambapa kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kusikiliza na
kwamba upande wa mashitaka upo tayari kuendelea.
Hata hivyo, Hakimu Mwambapa alisema hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Thomas Simba hayupo hivyo itaendelea kusikilizwa leo.
Mbali na Gwajima, washitakiwa wengine ni Askofu Msaidizi wa kabisa
hilo, Yekonia Bihagaze, mfanyabiashara George Mzava na mkazi wa Kimara
Baruti, Geoffrey Milulu.
Washitakiwa hao wanadaiwa walikutwa na begi likiwa na vitu mbalimbali
ikiwamo risasi 17 na bastola. Awali, katika utetezi wake, Gwajima
alidai kuwa Machi 27, 2015 alikuwa safarini kuelekea Arusha kwenye kikao
cha maaskofu, na aliondoka Dar es Salaam, Machi 26, 2015.
Alidai kuwa wakati alipokuwa njiani kuelekea Arusha aliona taarifa
kwenye mtandao wa kijamii kuwa Askofu Gwajima anatafutwa na Jeshi la
Polisi.
Alieleza kuwa alishangaa kuiona taarifa hivyo, hivyo akafika hadi
Arusha, lakini alishindwa kushiriki katika mkutano huo badala yake
alianza safari ya kurudi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kwenye
Kituo Kikuu cha Polisi Kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuripoti na
ndipo kesi hiyo ikafunguliwa na kuendelea kusikilizwa na watuhumiwa
kutakiwa kujitetea leo.
chanzo: zanzibar24.
Comments