GPSA yazichongea taasisi sugu zisizolipa.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu
Morogoro. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji ameutaka Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA) kuandaa orodha ya taasisi za umma zinazodaiwa na wakala huo na kuiwasilishe kwake.
Dk Kijaji alitoa agizo hilo hivi karibuni wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa GPSA, baada ya Mtendaji Mkuu wa Wakala huo, Jacob Kibona kueleza kuwa baadhi ya taasisi za umma zinawakwamisha kwa kutolipa madeni kwa wakati.
Pia, Kijaji aliwataka wakala huo kujadili na kutathmini utendaji wake kutokana na baadhi ya taasisi za umma kushindwa kununua vifaa kupitia kwao.
Awali, Kibona alisema walijadili bajeti na mpango kazi wa mwaka wa fedha 2017/18 ili kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyafanyakazi wa Serikali na Afya (Tughe), Lucas Mbele alisema suala la baadhi taasisi kushindwa kununua vifaa kwa wakala huo litajadiliwa kwa kina na kuhakikisha kila mtendaji anawajibika ipasavyo.     
chanzo:mwananchi.

Comments