Ametoa kauli hiyo katika hafla ya kutoa zawadi kwa shule 10 za msingi
na moja ya sekondari kwa kufanya vizuri kwenye mitihani ya darasa la
saba na kidato cha nne 2016.
Shule za msingi zilizopata zawadi na pongezi ni Tewe iliyokuwa ya
sita kimkoa na kuzawadiwa Sh 200,000, Chang’ombe Sh 150,000, Mkumba Sh
100,000, Mzundu Sh 82,000, Kwaragulu, Mbwewe, Kwamdani, Kwedikwazu
Magharibi, Kwedikwazu Mashariki na Chogo ambazo zote zilipata Sh 78,000.
DC Gondwe aliwataka wakuu wa shule na maofisa elimu kata kusimamia haki ya msingi ya wanafunzi kupata elimu wanayostahili.
Pamoja na kutoa pongezi kwa wanaofundisha na wadau wengine, amepiga
marufuku watoto walio na umri wa kuwepo shuleni kuchunga mifugo siku za
shule.
Aliwaonya wazazi na jamii ya wafugaji ambao wanakwamisha watoto
kupata haki yao ya msingi ya kupata elimu na kwamba sheria itachukua
mkondo wake kwa yeyote atakayebainika kwenda kinyume.
Aliwaeleza pia wazazi ambao wana watoto waliovuka umri wa kwenda shule kupelekwa kwa utaratibu wa MEMKWA.
Akizungumzia changamoto zinazowapata walimu, alisema atahakikisha
fedha zinazohusu madai ya walimu zinapofika halmashauri zinawafikia
walengwa kwa wakati uliopangwa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo,
William Makufwe alisema kukosekana kwa chakula cha kutosha shuleni,
utoro uliokithiri kwa baadhi ya wanafunzi, kutokuwajibika kwa baadhi ya
walimu na wazazi pamoja na upungufu wa walimu kunasababisha kushuka kwa
ufaulu wa wanafunzi.
Aliziagiza shule ambazo mpaka sasa hazina chakula kuhakikisha wanawapa wanafunzi chakula.
Aliwataka pia kusimamia mazao ya mihogo waliyopanda ili mazao hayo
yaweze kusaidia upatikanaji wa chakula shuleni na kuongeza kiwango cha
uelewa kwa wanafunzi.
Alitoa mwezi mmoja hadi kufikia Mei 4, mwaka huu kwa maofisa
watendaji kata, vijiji, walimu wakuu, wakuu wa shule na maofisa elimu
kata kuhakikisha kuwa watoto wanapata chakula cha mchana shuleni..
chanzo:Habarileo.
Comments