
Akitangaza bei hizo leo Meneja wa Mawasiliano wa Ewura nchini Tanzania , Titus Kaguo aliwaambia wanahabari kuwa petroli imeshuka kwa Sh 3 na itauzwa kwa Sh 2057 kutoka 2060, dizeli imepanda kwa Sh 12, kutoka Sh 1913 hadi 1925 na mafuta ya taa ni Sh 1958 kutoka 1952.
“Mabadiliko haya bei yametokana na bei za mafuta katika soko la dunia kubadilika sanjari na mfumuko wa bei na gharama za usafirishaji ikilinganishwa na mwezi uliopita,”amesema Kaguo
chanzo:zanzibar24.
Comments