
Hatua hii inatokana na marufuku iliyowekwa na serikali ya Rais
Donald Trump kuzuia baadhi ya raia wa mataifa yenye Waislamu wengi
kuzuru Marekani, pamoja na masharti mengine makali ya kiusalama.
Shirika hilo la ndege la Dubai limesema mabadiliko hayo yanatokana na kushuka kwa idadi ya watu wanaosafiri kwenda Marekani.
Mwezi
Machi, Marekani ilipiga marufuku vifaa vya kielektroniki ambavyo ni
vikubwa kuliko simu za rununu visibwebwe kwenye sehemu ya mizigo ya
ndege kutoka viwanja 10 vya ndege.
Viwanja hivyo ni pamoja na vya Dubai, na mataifa mengine ya Mashariki ya Kati, Afrika kaskazini na Uturuki.
Rais Trump pia alitia saini amri ya kuwazuia wahamiaji na raia
kutoka mataifa kadha yenye Waislamu wengi kutoka Mashariki ya Kati na
kaskazini mwa Afrika wasizuru Marekani.
Tayari kuna kesi zilizowasilishwa mahakamani kupinga marufuku hizo.
Msemaji
wa Emirates alisema: "Hatua za karibuni zilizochukuliwa na serikali ya
Marekani kuhusiana na kutolewa kwa viza za kuingia nchini humo, masharti
makali ya ukaguzi wa kiusalama na vizuizi kuhusu vifaa vya
kielektroniki kwenye mizigo ya ndege vimeathiri moja kwa moja nia ya
wateja kutaka kusafiri kwa ndege kwenda Marekani.
"Kwa
miezi mitatu iliyopita, tumeshuhudia kushuka pakubwa kwa idadi ya
wateja wanaowasilisha maombi ya kutaka kutumia ndege zetu kuingia
Marekani."
Rais wa Emirates Tim Clark alisema mwezi jana kwamba
idadi ya watu wanaotaka kwenda Marekani imeshuka kwa theluthi moja tangu
kutolewa kwa tangazo la Bw Trump.
Emirates imesema itapunguza safari za ndege kwenda
Fort Lauderdale na Orlando kuwa tano kila wiki kuanzia mwezi Mei, badala
ya safari moja kila siku.
Aidha, itapunguza safari kutoka mbili
kila siku kwenda Seattle na Boston hadi moja kila siku mwezi Juni, na
kwenda Los Angeles kwa kiwango sawa Julai.

chanzo:Bbc.
Comments