
Katika mahojiano na chombo cha habari cha Reuters amesema kuwa
angependelea mzozo huo kukabiliwa kidiplomasia lakini amesema hiyo
itakuwa vigumu kuafikia.
Bwana Trump alimpongeza mwenzake wa China Xi Jinping akisema amekuwa akijaribu kwa kila njia kuishinikiza Korea Kaskazini.
Awali
waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson alisema China
imeionya Pyongyang kutarajia vikwazo iwapo itafanya majaribio mengine
ya kinyuklia.
Wakati huohuo Korea Kaskazini imetoa kanda ya video ya propaganda ikionyesha itakavyoishambulia Marekani.
Kanda
hiyo inashirikisha ikulu ya Whitehouse na ndege ya kubeba ndege za
kijeshi inayokabiliwa na inakamilika na ikulu hiyo ikilipuka.
chanzo:Bbc.
Comments