Dk Shein amteua Bakari Naibu Mkurugenzi Mafuta na Gesi.



Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein
 Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amemteua  Ali Said Bakari kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo, Bakari alikuwa Ofisa Mwandamizi katika Idara ya Nishati, Zanzibar.
Dk Shein amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu Namba 53 cha katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, ambapo uteuzi huo unaanza leo.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na kusainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee leo tarehe 20 Aprili, 2017
 chanzo:mwananchi.

Comments