Dada mmoja apigwa panga la kichwa na kuporwa simu yake.

kichwa
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Agness amenyang’anywa simu yake na kupigwa panga la kichwa wakati akiwa amejipumzisha nje ya nyumba anayoishi maeneo ya Sogea Zanzibar.

Tukio hilo la kusikitisha limetokea juzi majira ya saa 5 usiku wakati dada huyo alipokuwa amelala nje ya nyumba aliyopanga huku akiwa ameshika simu yake mkononi ndipo alipotokea mtu asiyejulikana na kumpora simu hiyo kisha kumpiga panga la kichwa na kumsababishia maumivu makali.


Baada ya dada huyo kupiga kelele za kuomba msaada, majirani walitoka na kumkuta ameshika maeneo ya kichwa huku damu zikiwa zinamtoka kwa wingi na ndipo wakaamua kupeleka kituo cha polisi na baadae kumfisha katika hospitali ya Mnazi mmoja kwa ajilia ya matibabu na hadi sasa hali yake inaendelea vizuri .
 chanzo:zanzibar24.

Comments