Chande: watendaji wa mahakama hakikisheni mnamaliza kabisa mlundikano wa kesi.

JAJI Mkuu mstaafu, Mohamed Chande Othman amesema mahakama za Tanzania  ziko huru na angependa kuona watendaji wa mahakamani wakipambana ili kuhakikisha wanamaliza kabisa mlundikano wa kesi.
Katika mahojiano ya kwanza tangu astaafu aliyoyafanya  hivi karibuni, Jaji Othman alitoa mfano wa jinsi Mahakama ilivyoshughulikia kwa haraka kesi za uchaguzi wa mwaka 2015 uliokuwa na mvutano mkubwa.

Jaji huyo aliyefanya kazi za sheria nje na ndani ya nchi pamoja na taasisi kadhaa za kimataifa, alieleza kuwa kesi za uchaguzi za ubunge na udiwani zimemalizika bila malalamiko ya upendeleo.
Hata hivyo, anasema bado mahakama ina changamoto nyingi ikiwamo kila mkoa kuwa na Mahakama Kuu, kuongeza idadi ya mahakama za mwanzo na uboreshaji wa miundombinu huku akisikitishwa na baadhi ya mahakama kutokuwa na umeme.
 chanzo:zanzibar24.

Comments