
Japo Cosatu kinajulikana kuunga mkono chama tawala ANC, kimemshutumu
rais Zuma kwa kile wanachokitaja kuwa na uhusiano wa karibu mno na
familia moja ya jamii ya Wahindi huko Afrika Kusini, waitwao Gupta,
wanaodaiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika serikali ya Zuma.
Bw. Zuma na falimia hiyo ya Guptas, wamekana kufanya kosa lolote.
Wiki iliyopita chama chengine mshirika wa ANC The South African
communist party pia kilimtaka Bw. Zuma kung'atuka mamlakani kutokana na
kashfa tele zinazozidi kumuandama, madai ya makosa ya ufisadi.
Sarafu
ya Rand imekuwa ukiyumba yumba kutokana na malumbano hayo ya kisiasa
nchini Afrika Kusini hasa tangu kufutwa kazi kwa aliyekuwa waziri wa
fedha nchini humo Pravin Gordhan.
Rais Jacob Zuma amedhoofishwa kisiasa zaidi ya ilivyokuwa awali.
Wito wa Cosatu wa kumtaka kujiuzulu ni pigo kubwa kwa kiongozi huyo wa taifa.
Chama chicho cha wafanyikazi kimekuwa kikimuunga mkono dhidi ya wito wa kumtaka kung'atuka mamlakani.
Macho yote sasa yanaelekezwa katika kamati ya kazi ya chama cha ANC ambacho kinafanya mkutano.
Hatahivyo
licha ya uamuzi wowote utakaoafikiwa katika mkutano huo unaondelea,
mgawanyiko mkali uliopo katika chama hicho utazidi kati ya wale
wanaomuunga mkono Zuma na wapinzani wake.
Bwana Zuma anatarajiwa kuondoka mamlakani mwaka 2019 mwisho wa muhula wake wa pili kama rais wa taifa hilo.
Wiki iliopita,naibu wa rais Cyril Ramaphosa alipinga kufutwa kazi kwa bwana Gordhan.
chanzo:Bbc.
Comments