
Ngemela aliyasema hayo alipokua akizungumza Mjini Iringa katika mkutano na wanafunzi wa vyuo vikuu vyilivyomo mkoani humo ambao ni wananchama na pia viongozi wa chama hicho katika ngazi ya matawi na kata.
“Rais anapoteua kiongozi na kumpa dhamana ni kwamba anaona kuwa unahitajika, lakini inapofika mahali amekuondoa ujue mazingira yale huwezi kuyamudu na anakuokoa ili usipate laana. Baadhi ya viongozi wameondolewa madarakani, lakini wamebaki wakilalamika mitaani ovyo.” alisema Kanali Lubinga.
Lubinga alisema kuwa chama hicho sasa kimejikita kuhakikisha kuwa kinarejesha nidhamu na uwajibikaji ndani ya chama na serikali ili viongozi wote waliochaguliwa na kuteuliwa wafanye kazi kwa maslahi mapana ya taifa na wananchi.
chanzo:zanzibar24.
Comments