
Akizungumza Katibu wa Mkoa huo, Bi. Aziza Ramadhan Mapuri mara baada
ya kufanya ziara fupi katika Wilaya za Dimani na Mfenesini na
kuzungumza na wajumbe wa Kamati za Sekreterieti za wilaya 6hiyo kwa
lengo la kufanya tathimini ndogo juu ya maendeleo na kasoro zilizopo
katika uchaguzi huo.
Amesema ziara hiyo imekuja baada ya wanachama kutojitokeza kwa wingi
kuchukua fomu za kugombea nafasi kwa ngazi za mashina na matawi ya
jumuiya kutokana na kuwa na hofu iliyotokana na kutoelewa marekebisho ya
Katiba ya CCM ya mwaka 1977, juu ya kipengele cha kinachosema kazi za
muda wote kwa baadhi ya nafasi zinazogombewa.
Alisema wanachama wengi waliokuwa na nia ya kuchukua fomu
walitawaliwa na hofu ya kuwa endapo watajitokeza kuwania nafasi za ngazi
hizo watakuwa hawana fursa za kugombea nafasi zingine katika ngazi za
juu.
Aidha Katibu huyo alifafanua kwamba nafasi zilizotajwa kuwa ni za
muda wote ni zile za kiutendaji zikiwemo za Katibu na Mwenyekiti lakini
zingine zilizobaki zinaruhusiwa kushika nafasi zaidi ya moja na kwa
ngazi tofauti.
Pia alieleza kwamba chanzo cha kuwepo kwa ziara hiyo ni baada ya
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadalla kubaini
mapungufu katika mchato huo na kuagiza ngazi husika za chama na jumuiya
kutoa elimu na maelekezo ya kina juu ya changamoto hizo kwa viongozi wa
ngazi zote ili nao wawaelimishe wanachama katika maeneo husika.
” Tunatarajia kuwa baada ya kuongezwa muda wa uchaguzi wanachama wetu
wengi watajitokeza zaidi kuchukua fomu ili kupata viongozi wengi.”,
alisema Bi. Aziza.
Hata hivyo alipongeza maamuzi ya busara na hekima ya kujenga chama
yaliyofikiwa na Naibu Katibu Mkuu huyo kwa kuongeza muda wa uchukuaji wa
fomu ambapo kwa mujibu wa taarifa ya awali uchaguzi wa ngazi za chama
ulikuwa ufanyike April 17 hadi 31 mwaka huu lakini kwa sasa utafanyika
April 25 hadi 31 mwaka huu.
Kwa upande wa uchaguzi huo kwa ngazi ya Jumuiya za chama utafanyika
Juni 18 hadi 22 mwaka, na matarajio ya mkoa huo ni kuona muda uliobaki
unatumiwa vizuri na Wanachama wa chama hicho kwa kuchukua fomu kwa wingi
ili kupata viongozi na watendaji wenye sifa na vigezo vya kukiimarisha
chama na jumuiya.
chanzo: zanzibar24.
Comments