“Nakuagiza nenda ukafanye reform kubwa (mageuzi) kwenye eneo lako la
kazi, pale kuna changamoto kuwa na tumegundua kuwepo na dosari nyingi,”
alieleza Rais Magufuli alipomwapisha Dk Makakala, Februari 26, mwaka huu
baada ya uteuzi wake akitokea kuwa Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji Moshi
mkoani Kilimanjaro.
Alitoa mfano kuwa mwaka jana, Tanzania ilipata ugeni wa waumini wa
madhehebu ya Mabohora waliofanyia sherehe yao kubwa nchini. Alisema
sherehe hizo kwa kuwa zilikuwa za kimataifa wageni wapatao 32,000
waliingia nchini kuja kusherehekea sikukuu hiyo.
Alisema ukipiga hesabu ya kila mmoja ni wazi kuwa walilipa fedha za
kutosha; lakini cha ajabu ni kwamba alipouliza fedha kiasi gani
zilipatikana kutokana na ugeni huo mkubwa, hadi leo hajapatiwa hesabu
yoyote jambo linalodhihirisha kwamba kuna matatizo makubwa katika Idara
ya Uhamiaji.
“Kwa hiyo Kitengo cha Fedha pale Uhamiaji kuna matatizo makubwa,
nenda ukafanye mabadiliko.
Nimechagua mwanamke kwa kuwa naamini kwamba
wanawake ni waaminifu, kwa hiyo kufeli kwako ni kufeli kwa wanawake
wote, nenda ukafanye mabadiliko, usiogope sura, tutataka ukafanye total
reform (mageuzi makubwa), not partial reform (mageuzi nusu),” alisema
Rais Magufuli.
Kabla ya mabadiliko makubwa ya jana, Dk Makakala aliteua makamishna
sita ambao ni Peter Chogero ambaye ni Kamishna wa Divisheni ya Fedha na
Utawala, Samwel Magweiga (Kamishna wa Divisheni ya Udhibiti na Uongozi
na Mipaka), Gerald Kihiga (Kamishna wa Divisheni ya Pasipoti na Uraia),
Musanga Etimba (Kamishna wa Divisheni ya Hati za Ukaazi na Pasi) na
Hannerole Manyanga ambaye ni Kamishna wa Divisheni ya Sheria.
Lakini jana, Dk Makakala alitangaza mabadiliko mengine makubwa ambayo
yameshuhudia Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Sixtus Nyaki aliyekuwa Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Mwanza akihamishiwa Mkoa wa Simiyu wakati aliyekuwa
Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Selemani
Kameya amehamishiwa Tabora.
Taarifa iliyotolewa na Kamishna Jenerali huyo inaonesha kuwa Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumsio Achacha
amehamishiwa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Manyara,
Naibu Kamishna Peter Kundy amehamishiwa Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi
ya Kamishna Msaidizi, Ali Mohamed ambaye amehamishiwa kuwa Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Arusha.
Aidha, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mkemi Seif ameteuliwa kuwa Mkuu wa
Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Muhsin
Abdallah Muhsin ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini
Unguja, Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Said Omary Hamdani ameteuliwa kuwa
Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi na Naibu Kamishna wa Uhamiaji
Othman Khamis Salum ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mjini Magharibi
Unguja.
Pia baadhi ya wakuu wa Uhamiaji wa mikoa wamebaki katika vituo vyao
vya kazi vya awali akiwemo Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro, Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Safina Muhindi, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Lindi,
Naibu Kamishna wa Uhamiaji George Kombe, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa
Ruvuma, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Hilgaty Shauri, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa
wa Singida, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Faith Ihano na Mkuu wa Uhamiaji
Mkoa wa Mara, Naibu Kamishna Fredrick Kiondo.
Wamo Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Abdallah Towo (Kagera) na Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Anastazia Ngatunga (Shinyanga). Taarifa hiyo
iliongeza kuwa Dk Makakala pia amewateua viongozi wa Uhamiaji wa mikoa
wapya katika baadhi ya mikoa nchini ambapo Naibu Kamishna wa Uhamiaji,
Mary Palmer ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam,
Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Plasid Mazengo (Pwani), Mrakibu Mwandamizi
wa Uhamiaji James Mwanjotile (Mtwara), Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hope
Kawawa (Iringa), na Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Hosea Kagimbo
(Njombe).
Wengine ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji Rashid Magetta (Songwe), Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Carlos Haule (Rukwa), Naibu Kamishna wa Uhamiaji
Julieth Sagamiko (Manyara), Naibu Kamishna wa Uhamiaji Albert Rwelamila
(Kilimanjaro) na Naibu Kamishna wa Uhamiaji Paul Eranga (Mwanza).
Naibu Kamishna wa Uhamiaji Crispin Ngonyani (Tanga), Naibu Kamishna
wa Uhamiaji Shaaban Hatibu (Katavi), Naibu Kamishna wa Uhamiaji Remigius
Pesambili (Kigoma) na Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Novaita Mrosso
(Mbeya).
Aidha, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Bakari Mohamed Ameir ameteuliwa
kuwa Mkuu wa Kituo cha Uhamiaji cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume, Zanzibar na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji
Fulgence Mutarasha kuwa Mkuu wa Uhamiaji Kituo cha Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Bosi mpya aifumua idara ya Uhamiaji Inatoka Uk. 1 Wapinzani wavurunda
Na Magnus Mahenge, Dodoma OFISI ya Bunge imeshindwa kuteua wagombea wa
vyama vya upinzani kwa ajili ya uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki
(EALA) unaofanyika leo baada ya kukiuka kanuni za uchaguzi huo na
vimepewa hadi leo saa saba mchana kurekebisha upungufu kwenye fomu
mbalimbali za wagombea.
“Kutokana na upungufu huo, msimamizi wa uchaguzi nimeshindwa kuteua
wagombea wa kundi hilo, hivyo nimeviandikia vyama vyenye haki ya
kugombea kuvitaka kurekebisha upungufu ulioainishwa na kuwasilisha
majina na nyaraka zinazohitajika ofisini kwangu Dodoma Aprili 4, mwaka
huu kabla ya saa saba mchana,” alisema Katibu wa Bunge, Dk Thomas
Kashililah.
Dk Kashililah ambaye ni Msimamizi wa Uchaguzi huo, alisema Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF)
havikuzingatia masharti ya Ibara ya 50 ya Mkataba wa Kuanzishwa Jumuiya
ya Afrika Mashariki (EAC), inayotaka theluthi moja ya wabunge tisa
izingatie jinsia zote mbili.
CCM ndicho chama pekee ambacho kimewasilisha orodha ya nyaraka
zinazoonesha wagombea wake wote wamekidhi vigezo na masharti ya uchaguzi
wa kuwa wabunge wa EALA. Alisema Chadema haijazingatia jinsia ili
kuwezesha utekelezaji wa masharti ya kifungu namba 4 (4) cha sheria ya
wajumbe wa EALA ya angalau theluthi moja ya wajumbe zioneshe jinsia zote
mbili.
Pia alisema haijawasilisha fomu za wagombea, orodha ya waombaji haipo
na fomu za matokeo ya kura zilizopigwa hazipo.
Hata hiyo, Ofisa Habari
wa Chadema, Tumaini Makene alidai hakuna utaratibu wowote uliokiukwa kwa
wao kuteua wagombea wa nafasi za ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki
isipokuwa msimamizi wa uchaguzi, Dk Kashililah ameamua kuja na utaratibu
wake anaoujua mwenyewe, hivyo walitarajia kutoa msimamo wao jana jioni.
“Hakuna taratibu zilizokiukwa katika kuteua wagombea wetu wa kugombea
ubunge wa EALA, isipokuwa msimamizi wa uchaguzi, Dk Kashililah ameamua
kutoa msimamo wake mwenyewe, sisi tutatoa msimamo wetu jioni ya leo
(jana),” alidai Makene.
Naye Kaimu Katibu Mkuu wa CUF, Magdalena Sakaya
amesema chama hicho kina imani na Spika Job Ndugai kuwa atafuata sheria
na kanuni za uchaguzi kwa kutambua CUF ni moja na haina vipande vipande
hasa katika suala la wagombea wa Afrika Mashariki.
Alisema wanaamini Spika atatenda haki katika suala la wagombea ubunge
wa Bunge la Afrika Mashariki kwa kuamini CUF ni moja na haiko vipande
vipande. Uteuzi ndani ya CUF haujazingatia jinsia ili kutekeleza
masharti ya kifungu namba 4 (4) sheria ya uchaguzi wa wajumbe wa Bunge
hilo ambayo inataka kati ya wabunge tisa ioneshe uwepo wa jinsia zote.
Alisema fomu za uteuzi wa wagombea zimewasilishwa na mamlaka mbili
tofauti, wagombea wawili hawana uthibitisho wa uraia, orodha ya waombaji
haipo kwa mgombea mmoja, fomu ya matokeo ya kura kwa wagombea wote
haipo na fomu ya mahudhurio kwa mgombea mmoja haipo.
“Uteuzi wa wagombea wa kundi C wa vyama vya upinzani utafanyika
Aprili 4, mwaka huu, wakati wowote kuanzia saa saba kamili mchana mara
baada ya kupokea na kuchambua nyaraka zitakazowasilishwa kwangu na vyama
husika,” alieleza Dk Kashililah.
Kutokana na mamlaka aliyopewa, Msimamizi wa Uchaguzi alitangaza na
kutoa taarifa kwa umma kwamba waliokidhi vigezo na masharti ya kuteuliwa
kugombea kwenye uchaguzi wa wajumbe wa EALA uliopangwa kufanyika leo.
Wagombea waliokidhi vigezo kutoka kundi A la wanawake ni Happiness
Lugiko (CCM) na Zainabu Kawawa (CCM), kundi B la wanaume Tanzania Bara
ni Adam Kimbisa, Anamringi Macha, Charles Makongoro, Dk Ngwalu Maghembe,
Fancy Nkuhi na Happiness Mgalula na wagombea wa kutoka Zanzibar ni
Abdullah Husna Makame, Maryam Ussi Yahya, Mohamed Yusufu Nuhu na Rabia
Abdallah Hamid.
Wagombea wa vyama vya upinzani ambao hawajakidhi vigezo ni Ezekiel
Wenje na Lawrance Masha (Chadema), Habibu Mohammed Mnyaa, Sonia Jumaa
Magogo, Thomas Malima na Twaha Taslima (CUF).
Wengine ni Nderakindo Perpetua Kessy (NCCR-Mageuzi) na Profesa Kitila
Mkumbo (ACT-Wazalendo), Majina ya wagombea hao yaliwasilishwa na vyama
vyao tangu Machi 30, mwaka huu kabla ya saa 10 jioni kama masharti ya
kanuni ya 5 (4) ya nyongeza ya tatu ya kanuni za kudumu za Bunge toleo
la Januari 2016.
Baada ya hatua hiyo, uchambuzi ulifanyika kwa kuzingatia ibara ya 50
ya mkataba, ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya mwaka 1977, sheria ya
uchaguzi wa wa wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) na kubaini
upungufu kwa vyama hivyo.
Dk Kashililah aliwapongeza wagombea waliojitokeza katika nafasi
mbalimbali wanaofikia 505, CCM (471), Chadema (17), CUF (8),
NCCR-Mageuzi (3) na ACT-Wazalendo (6). Wagombea hao walichujwa na vyama
vyao na kubakiza majina 20 kugombea ambao ni CCM (12), Chadema (2), CUF
(4), NCCRMageuzi (1) na ACT-Wazalendo (1).
Katika wagombea hao, wanaume ni 12 na wanawake ni wanane, CCM
(wanawake 6 na wanaume 6), Chadema mwanamke mmoja na wanaume wawili, CUF
mwanamke mmoja na wanaume watatu, NCCR-Mageuzi mwanamke mmoja na hakuna
mwanamume na ACT-Wazalendo hakuna mwanamke na mwanamume ni mmoja.
Uchaguzi huo ukikamilika watapatikana wabunge tisa wa kuwakilisha
Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki lenye makao yake makuu Arusha.
Katika orodha hiyo, wabunge wa CCM watakuwa sita na wabunge wa upinzani
watatu.
Shughuli zikiendelea kama kawaida katika Kituo Kikuu cha Mabasi ya
Mikoani Ubungo, Dar es Salaam jana baada ya mgomo uliokuwa ufanywe na
wasafirishaji wa abiria kupatiwa ufumbuzi baada ya mazungumzo baina ya
serikali na wamiliki wa mabasi nchini. (Na Mpigapicha Wetu.
chanzo:Habarileo.
Comments