Baraza la manispaa kula sahani moja na wauza biashara wanaokiuka masharti ya usafi.

barazaBaraza la Manispaa Zanzibar limesema  halita  wafumbia macho wauza biashara  ndogondogo wakiwemo mama ntilie  na wauza  vioksi vya chips watakao kiuka masharti waliyopewa  hususani katika kipindi hichi cha mvua za masika zinazoendelea ili kuepusha miripuko ya maradhi ya Kipindupindu hapa Zanzibar.

Akizungumza na Zanzibar24 Afisa  Mazingira wa baraza hilo Jaku  Abdalla Jaku amesema katika kipindi cha mvua maradhi ya miripuko hujichomoza kutokana na mazingira kuwa machafu hivyo ili kuepusha na kunusuru afya za wananchi mfanyabiashara watakao
gundulika  anakwenda kinyume katika kudhibiti mazingira   maeneo yao ya biashara yatafungiwa bila ya kumuonea muhali.

Hata hivyo amesema baraza la manispaa limeanza kufanya ukaguzi nyumba kwa nyumba ili kuwachukulia hatua za kisheria wananchi waliokuwa hawana  karo za kutunzia maji machafu kwani  maji hayo huhatarisha afya kwa jamii.

Aidha amesema  wamekuwa wakitoa   elimu kwa wananchi lakini  baadhi yao imeonekana   wanaizarau   elimu hiyo ametoa  wito kwa jamii kuwa na  mashirikiano  katika kudhibiti mazingira ili kunusuru  majanga yanayoweza kuepukikana pamoja na kuwacha kutupa taka katika mitaro ya maji machafu.

Jumla ya wafanyabiashara 20 wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani kutokana na kukiuka masharti ya afya waliyopewa.
chanzo:Zanzibar24

Comments