
Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa kitengo cha mabadiliko tabia nchi
kisiwani Pemba, Ali Abdi Mohamed alipokuwa akifungua mkutano wa wazi kwa
wananchi, wenye lengo la kuwahamasisha upandaji miti na uhifadhi wa
mazingira, ili kupunguza kasi ya mabadiliko tabia nchi.
Alisema kisiwa cha Makoongwe, ni miongoni mwa visiwa vidogo vidogo
ambavyo navyo, zimeshaanza kukumbwa na athari za mabadiliko tabia nchi,
sasa lazima wananachi wenyewe wajipange haraka, badala ya kusubiri
wafadhili.
Abdi alieleza kuwa, kukatazana kuchukua mchanga pembezoni mwa fukwe,
kutokata miti ovyo, kuacha kuchimba mashimo kwenye mikoko ni miongoni
mwa hatua, ambazo wananchi hao wa kisiwa cha Makoongwe wanaweza
kuzichukua pasi na fedha za mfadhili.
“Kila anaekikumbuka kisiwa cha Makoongwe miaka 25 iliopita, sasa
akipata kukitembelea miaka hii, anaweza kuona jinsi kisiwa hicho,
kinavyomegwa na maji ya bahari, ndio maana tunahimizana tuchukue hatua
sasa’’,alishuari.
Kuhusu kisiwa Panza, ambao wananchi wamepata mradi wa kupunguza kasi
ya mabadiliko tabia nchi, ambao wanatarajia kupanda miti ya aina mbali
mbali 400,000 amewataka wananchi kuitunza, ili isaidie na kisiwa chao.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mazingira wilaya ya Mkoani, Rashid
Abdalla Salum, alisema hali ya kisiwa cha Makoongwe, imeanza kutisha
kutokana na kila eneo kuingia maji ya bahari.
“Kila eneo sasa lina mto wa maji ya bahari, lakini na sisi wananchi
wa kisiwa hichi, tumekuwa hanasababisha kwa kuchimba mchanga kwenye
mashamba ya wakulima na hata pembezoni mwa fukwe’’,alifafanua.
Mapema Katibu wa Jumuia ya Sanaa, Ealimu ya Ukimwi na Mazingira
JSEUMA, Juma Ali Mati, alisema kupitia mradi wa Kupunguza kasi ya
mabadiliko tabia nchi waliopata, wanakusudia kupanda miti kwenye hekta
200.
Aidha Mati alisema wananchi 110 wameshapewa taaluma ya kupambana na
kasi ya mabadiliko tabia nchi, wakiwemo wa Kisiwapanza, Makoongwe,
Michenzani, Chokochoko, Kangani, Mwambe na Mtambile.
Wananchi wa kisiwa hicho, wamepongeza hatua ya wao kukumbushwa wajibu
wao kama wananchi, katika kupambana na kasi ya mabadiliko tabia nchi.
Ahmed Ali Siasa alisema awali walikuwa hawajui wao kama wananchi nafasi yao katika kupambana na kasi ya mabadiliko tabia nchi.
“Sasa baada ya elimu mliotupa na sisi wananchi tumeshajua wajibu
wetu, lazima tuhamasishane maana athari zake humkumba kila
mmoja”,alifafanua.
Jumuia ya sanaa, elimu ya ukimwi na mazingira JSEUMA ya kisiwa panza,
imeshapanda miti kwenye maeneo ya Kitunga ndege, Maduuni ambapo
wakulima 50 wamerejea tena kwenye bonde hilo, baada ya kukihama kutokana
na kuvamiwa maji ya bahari.
chanzo: zanzibar24.
Comments