
Hayo yalisemwa jijini hapa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu,
Kamishna wa Polisi, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa
habari.
Kamanda Sirro alisema tukio hilo lilitokea Machi 31, mwaka huu saa
saa nne usiku katika maeneo ya Sinza Shekilango jijini Dar es Salaam.
Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya ufuatiliaji wa taarifa ya
tukio la mauaji ya mwanamke aliyejulikana kwa jina la Samira Masoud (34)
aliyeuawa kwa kuchinjwa Machi 7, huko Kibamba na kisha mwili wake
kuwekwa katika doo kubwa la maji huku ukiwa umeharibika vibaya.
Aliongeza kuwa mtuhumiwa huyo katika mahojiano, amekiri kufanya
mauaji ya mwanamke huyo na kusema sababu kubwa ilikuwa ni wivu wa
kimapenzi baada ya kumfumania mpenzi wake akiwa chumbani na mwanamume
mwingine ambaye hata hivyo mwanamume huyo alitoroka.
Alisema awali mtuhumiwa huyo aliwatumia ndugu wa marehemu ujumbe
mfupi wa maandishi kwa kutumia namba ya simu ya marehemu ukisema:
“Nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu itaozea ndani.”
“Mtaweza kuona ni ukatili wa namna gani uliofanywa na kijana huyu,
hata kama mtu umemshika ugoni hupaswi kufanya tukio kama hili la
kinyama,” alisema Kamanda Sirro na kuongeza kuwa upelelezi wa tukio hilo
unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa
hatua zaidi.
chanzo: zanzibar24.
Comments