
Akiongea na waandishi wa habari, Dkt Mwakyembe amesema tukio hilo linaweza kuwa limefanywa na watu wachache kwaajili ya kuvuruga mambo.
“Hawa ni stars, hawa ndio wanainbrand Tanzania. Huyu ni bendera ya Tanzania, siwezi kukubali tukachezeachezea watu hawa kwasababu zozote zile, ndio maana nasema tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha kwamba tunaviruhusu vyombo vya upepelezi ambavyo vitafuatilia kwa ukaribu sana tupate majibu ya kile kilichotokea,” amesema Mwakyembe.
Dkt Mwakyembe amesisitiza kuwa wizara yake ipo kwaajili ya wasanii na itawalinda kwa namna yoyote na kwamba pale watakapoona hatari yoyote wasisite kumjulisha.
Amesema anachosubiri ni majibu ya upepelezi ulioanza na kwamba atahakikisha anaupata na kuusema bungeni wakati anawasilisha bajeti yake.
chanzo:zanzibar24.
Comments