
Tukio hilo lilitokea baada ya ng’ombe wake waliokuwa wakichungwa na
mkewe kukamatwa na mdeni wake ili kumshinikiza amlipe deni hilo.
Magige alisema, Aprili 5 akiwa safarini alipigiwa simu kuwa mifugo
yake imekamatwa na uongozi wa Kijiji na alitakiwa kwenda kuikomboa,
baada ya hapo alisitisha safari na kurejea nyumbani, alikwenda kwa
Mwenyekiti wa Kijiji, Nuru Magacha alimweleza kuwa mifugo yake ipo na
anadaiwa sh 300,000.
Magige alisema muda mfupi baadaye palipigwa mayowe kuashiria hatari
huku akiwa hajui kinachoendelea, wananchi walikusanyika na ndipo kijana
mmoja alimkata mkono wa kushoto kwa panga na kuucha ukining’inia.
chanzo: zanzibar24.
Comments