Jaji Joaquine De-Mello alitoa hukumu hiyo jana katika kesi namba
9/2016 katika kikao cha Mahakama Kuu inayoendesha vikao vyakeMahakama ya
Wilaya Tarime. Awali, Mwanasheria wa Serikali, Harry Mbogoro alidai
kuwa Agosti 17, 2015 saa 7 usiku Wankyo akiwa katika Hoteli ya NK
iliyopo mjini Tarime akiwa na mpenzi wake wakila chakula na vinywaji,
alifika askari wa JWTZ, Elias akiwa na wenzake wawili na kutaka
kumchukua mwanamke aliyekuwa naye Jacob.
Alidai alimshambulia kwa kumpiga ngwala na kumwangusha chini, na
mtuhumiwa alitaka kujiokoa akiwa ameangushwa chini huku akiwa na silaha
yake na risasi iliyokuwa ndani ya bastola yake anayomiliki kihalali,
ilifyatuka na kumjeruhi Elias aliyekimbizwa Hospitali ya Wilaya Tarime
kisha kuhamishiwa Hospitali ya Bugando jijini Mwanza ambako alifariki
wakati akipatiwa matibabu.
“Mtuhumiwa baada ya tukio hilo usiku huo alifika Kituo cha Polisi
Tarime akiwa na majeraha aliyopigwa wakati wa ugomvi na askari hao na
kupewa PF 3 ya kupatiwa matibabu na kusalimisha silaha yake na baadaye
kuwekwa chini ya ulinzi na kushitakiwa kwa kuua bila kukusudia amekaa
rumande kwa miezi sita na kupewa dhamana,” alidai mwanasheria huyo wa
serikali.
Wakili wa upande wa utetezi, Deus Mgengeri alimtetea mteja wake kuwa
mtuhumiwa walikuwa hawana chuki wala fitina yoyote na marehemu, bali ni
ugomvi uliotokana na kugonganishwa na mwanamke na kumshambulia Tumaini
kwa kumpiga ngwara na kumuangusha chini akiwa na wenzake ambapo
mtuhumiwa alitaka kujiokoa na kipigo kutoka kwa askari hao.
Hana rekodi mbaya ya makosa ya jinai na ni kosa lake la kwanza, hivyo
akaomba Mahakama kumpa adhabu ndogo mteja wake. Jaji De-Mello
alimhukumu mshitakiwa kwenda jela mwaka mmoja ili iwe fundisho kwa watu
wengine.
chanzo:Habarileo.
Comments