Afariki Dunia kwa kuzama kwenye daraja.

Related imageMtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Abduli Haji Adam amefariki Dunia baada ya kuzama katika daraja la Shuweni lililopo kisongoni ndani ya Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kwa mujibu wa taarifa zilizosibitishwa na kamanda wa polisi Bi Hasina Ramadhan Taufik amesema kuwa kabla ya kifo chake mtu huyo alikuwa katika shuhuli zake za kilimo na baada ya kumaliza kulima aliamua kwenda kukoga katika daraja hilo ndipo alipoanguka na kuzama na kufariki Dunia.

Hivyo kamanda wa huyo alitoa wito kwa jamii kuwa makini na mito na maziwa pamoja na makaro ambapo mengi yamejaa hasa katika kipindi hichi cha mvua zinzoendelea.
chanzo:zanzibar24.

Comments