Zanzibar hatarini kukosa umeme kutokana na deni la bilioni 121.

Rais Dr. John Magufuli jana aliiagiza (Tanesco) kuwakatia umeme wateja wote wenye madeni makubwa  ikiwemo serikali ya Zanzibar kutokana marimbikizo ya madeni yanayodaiwa.
Alisema kuwa  Zanzibar  kupitia shirika la umeme za Zanzibar (Zeco), imekua ikiongoza kwa deni la Tanesco kiasi cha shilingi bilioni 121 za Tanzania jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya TANESCO.

Akizungumzaalipokwenda kuweka jiwe la msingi kwenye kituo kipya cha Tanesco mkoani Mtwara, rais Magufuli alizitaka  tasisi zote za umma kulipa madeni yao la sivyo zitakatiwa umeme haraka bila kuogopwa.
“Msiogope mnapaswa kukata huduma hii kwa taasisi yoyote ambayo hailipi bili zake.Nataka kumwambia waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwamba umeme unapaswa kukatwa hata Ikulu. Nikilala gizani, halafu maafisa wa Ikulu ambao hawajalipa watawajibika na sio wewe. Una hakikisho langu kwa hili.
Pesa za kulipa bili kawaida hutolewa kwa wizara zetu, lakini badala yake hupelkwa kwingine
.”ninaambiwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haijalipa Sh121 billion. Ninyi (Tanesco) si wanasiasa…mnapaswa kuzingatia majukumu yenu ya kitaaluma…kata huduma ya umeme.Nimesema hata kama ni Ikulu , polisi, jeshi ama shule , hakuna mwenye deni anaepaswa kuachwa . 
Ni kwa njia hii tu tunaweza kuhakikisha kwamba pesa zilizotengewa wizara kwa ajili ya umeme zinatumiwa kama ilivyopangwa ili Tanesco iweze kuendesha kazi zake na kushughulikia matatizo ya uhaba wa umeme. 
”Tanesco haiwezi kuboresha huduma kwa sababu ya madeni ya serikali yasiyolipwa”.
Nae  Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa pili wa rais , Bwana Mohammed Aboud, alisema kuwa Maagizo ya rais Magufuli yako wazi, Madeni lazima yalipwe na yatalipwa na mipango inafanyika kwa ajili ya kuliwezesha shirika la Zeco kulipa madeni ya Tanesco.
” Tumeanza mchakato wa kuhakikishwa suala hili linatatuliwa.Pia tumeiagiza Zeco kuacha kulimbikiza madeni mapya”.
 chanzo:zanzibar24.

Comments