
Amesema kwa sasa imekuwa kama fashion kwa RCs na DCs kukamata watumishi wa umma hasa madaktari na kuwaweka ndani, vitendo vinavyopelekea kushusha morali ya kazi.
Ameongeza kuwa ameshakubaliana na Waziri wa TAMISEMI kuhusu kuwaelekeza Wakuu wa Wilaya na Mikoa mipaka yao ya kazi ili wasiingilie kazi na taratibu nje ya majukumu yao.
Agizo hili limekuja siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kumuweka ndani DMO wa Singida na kusababisha daktari huyo kuandika barua ya kujiuzulu na kuacha kazi.
chanzo:zanzibar24.
Comments