Waziri Castico aungana na wanawake katika shamrashamra za siku ya wanawake Duniani.

Waziri wa kazi,Uwezeshaji,Vijana,Wazee,Wanawake na Watoto Moudline Cyrus Castico amesema serikali imedhamiria kuweka mikakati ya kuimarisha hali ya ustawi wa wanawake pamoja na kutoa  fursa mbalimbali za kumuwezesha wanawake kiuchimi.


Akizungumza na Waandishi wa habari ikiwa ni shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo inatarajia kuadhimishwa kesho Jumatano, amesema  wanawake wamepewa kipaumbele katika fursa mbalimbali za maendeleo ili kuhakikisha wanainuka  kiuchumi kwa lengo la kujikimu kimaisha.


Hata hivyo amesema licha ya kujitokeza vitendo vingi vya udhalilishaji kwa wanawake na watoto ambavyo vinawarudisha nyuma wanawake kimaendeleo  lakini serikali haitokaa kimnya katika kupambana na hali hiyo ili kumkombea mwanamke katika maisha duni na kumfikisha katika maendeleo imara.


Wakati huo huo Wanawake kutoka Wilaya mbalimbali Unguja walifanya kongamano la kuadhimisha siku ya wanawake duniani akiwemo Mtumwa Ali na Arafa Juma Faki wamesema ili ya kujiinua kiuchumi kwa kuchukua mikopo mbalimbali ya kimaendeleo ila wanarudishwa nyuma na kushindwa kupata soko la kuuzia bidhaa zao na kutojua elimu ya biashara.

Siku ya wanawake duniani imekuja baada ya wanaharakati wa viwanda walivoandamana kupiga kuonewa waliokuwa wakifanyiwa na waajiri wao  mwaka 1859 ambapo baada ya kuasisiwa umoja wa kimataifa mwaka 1945 baraza la umoja wa kimataifa ilitanga kila ikifika tarehe 8 March kila mwaka ni siku ya wanawake duniani na kwaupande wa zanzibar imeaza kuadhimisha tokea mwaka 1991 na Ujumbe wa mwaka huu ukiwa ni “Imarisha fursa za ajira kwa kumuwezesha wanamke kiuchumi”.

chanzo:Zanzibar24

Comments