
Wakichangia hoja binafsi iliyowasilishwa na Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae Mohammed Said Mohammed
wajumbe hao ni Zulfa Mmaka Omar,Nadir Abdul-latif,Hassan Khamis Hafidh na Hussen Mohammed Makungu wamesema endapo serikali itafanya kazi kwa kushirikiana na jamii pamoja na wajumbe hao maazimiyo hayo yataweza kufanikisha katika kuwatia mbaroni waingizaji,wasambazaji na watumiaji wa madawa ya kulevya.
Akisoma maazimio yaliyoungwa mkono na wajumbe wa baraza hilo Mohammed Said Mohammed Dimwa amesema Serikali ihakikishe inasimamia vyema sheria namba 9 ya 2009 ya kuzuia biashara haramu ya dawa za kulevya bila ya kumuonea mtu muhali ili kulinusuru taifa.
Jumla ya kesi 569 zilizofunguliwa za madawa ya kulevya kwa mda wa miaka minne iliyopita kutoka 2013 hadi 2016.
Chanzo:Zaznibar24
Comments