Watakao pinga agizo la mkuu wa wilaya kuchukuliwa hatua.

Image result for mbwaMKUU wa Wilaya ya Micheweni, Mh  Abeid Juma Ali, amesema kuwa, atawachukulia hatua wale wote watakaokiuka  agizo la kuwapeleka mbwa kuchanjwa kwa makusudi  na bila ya sababu zisizo eleweka kisheria.

Mh, Mkuu wa  Wilaya ameyasema  hayo wakati alipokuwa, akizindua zoezi la utoaji wa chanjo ya kichaa cha Mbwa huko Shehia ya Konde, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba. 

Mkuu wa Wilaya amesema kuwa, kuna watu wanatabia ya kudharau maagizo ya Serikali wakiyahusisha na siasa jambo ambalo ni kinyume ya malengo yaliokusudiwa na kupelekea madhara makubwa kwa jamii.

Akitoa maelezo mafupi juu ya umuhimu na malengo ya njanjo za Kichaa cha mbwa. 

Afisa Mipango wa Idara ya Maendeleo ya Mifugo Pemba
Suleiman Hamadi Hija, amesema kuwa, lengo la kutoa huduma hiyo ni kutokomeza ugonjwa wa Kichaa cha Mbwa ambao unaathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya Wanadamu na Wanyama kiujumla.

Afisa mipango huyo amesema kuwa, kumekuwa kukiongezeka matukio ya watu na Wanyama kuumwa na mbwa siku hadi siku katika Wilaya Micheweni kutokana na mwitiko mbaya wa jamii katika kipindi cha uchanjaji wa
Mbwa mwaka uliopita.

Nae Mfugaji wa Mbwa, Kutoka Sehiya ya Konde, Sadam Said Ali, alisema kuwa Serikali imewasaidia kwa hatua kubwa kuwapatia huduma ya chanjo ya kichaa cha Mbwa, bila ya malipo, ili kusaidia usalama wa afya zao.

Huduma ya utoaji wa chanjo ya Kichaa cha Mbwa ambayo ilifanyika mwezi Septemba mwaka jana katika Wilaya zote nne kwa Pemba, ni Wilaya ya Micheweni Pekee ambayo imekuwa ikiripotiwa matokeo ya watu kuumwa na Mbwa kuanzia Januari hadi kufikia idadi ya watu 38, Machi 13 Mwaka huu, kutokana na kutoitikia wito kikamilifu kupata huduma hiyo.

Comments