Wanawake wa jamii ya wafugaji wa Barbaig wamelalamikia vitendo vya udhalilishaji wanavyofanyiwa na Polisi.

Wanawake wa jamii ya wafugaji wa Barbaig wamesema wamelalamikia vitendo vya ubakaji hadi kufa, kuibiwa mifugo, kuchomewa mabanda na waume zao kuuawa.

Wameyasema hayo mbele ya viongozi wa serikali katika mkutano wa kutafuta suluhu ya maiti zilizoachwa kuzikwa sababu ya tofauti ya polisi na wabarbaig hao.


Katika mkutano huo, polisi wametuhumiwa kuwa wamekuwa wakiiba unga wa mahindi kwenye mabanda ya wafugaji, kuiba maziwa, simu na vitu vyenye thamani wanapovamia na kuchoma nyumba za wafugaji.

Aidha Wabarbaig hao wameomba kila kiongozi wa serikali anapoenda kuwaondoa wafugaji awe anawatajia eneo mbadala na si kuwafanyia ukatili.

chanzo: zanzibar24.

Comments