
Akizungumza katika Mafunzo ya asasi za kiraia juu ya kukabiliana na
mabadiliko ya tabianchi,
Mratibu wa Jumuiya ya ZACCA Soud Mohammed Juma
amesema kutokana na utafiti uliofanywa imeonekena maeneo mengi ya
Zanzibar yameathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa hasa katika
maeneo ya kilimo kwa kuvamiwa na maji ya bahari, maji ya visima kugeuka
ya chumvi pamoja na kuongezeka kwa gesi joto.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kutokana na hali hiyo basi ipo
haja kwa serikali kwa kushirikiana na asasi za kiraia kudhibiti
mabadiliko hayo kwa kuchukua hatua za haraka kwani elimu tayari
imeshatolewa lakini bado jamiii haijawa tayari kushirikiana na kuendelea
kufanya vitendo vya uharibifu wa mazingira.

chanzo:Zanzibar24
Comments