Wanamgambo wa al Shabab wauawa kusini mwa Somalia.

Wanamgambo kadhaa wa kundi la kigaidi la al Shabab wameuawa katika oparesheni iliyofanywa na jeshi la Somalia katika maficho ya kundi hilo kusini mwa nchi hiyo.

Duru za kiusalama za Somalia zimetangaza kuwa jeshi la nchi hiyo jana Ijumaa lilitekeleza oparesheni karibu na mji wa bandari wa Kismayo katika jimbo la Jubaland na kuwauwa wanamgambo sita wa kundi la al Shabab.


Duru hizo zimesisitiza kuwa oparesheni hiyo ya jeshi ambayo imeanza kwa lengo la kuharibu maficho ya kundi la al Shabab itaendelea katika siku zijazo. 

Kundi la kigaidi la al Shabab linaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya raia na askari usalama huko Somalia licha ya jeshi la nchi hiyo kuendesha operesheni ya kuwaangamiza wanamgambo wa kundi hilo nchini humo.

Kundi la al Shabab ambalo lilikuwa likiyadhibiti baadhi ya maeneo ya katikati na kusini mwa Somalia, mwaka juzi wa 2015 lilipoteza udhibiti wa miji mikubwa na hivi sasa linadhibiti maeneo kadhaa katika baadhi ya miji ya Somalia.
CHANZO: parstoday.

Comments